SikilizaTogolani Profile
SikilizaTogolani

@SikilizaTogolan

Followers
59,489
Following
0
Media
999
Statuses
1,012

Kila Mtu kwa KARAMA yake, KADRI yake na KUDRA yake!

Republic of Korea
Joined November 2021
Don't wanna be here? Send us removal request.
Explore trending content on Musk Viewer
@SikilizaTogolan
SikilizaTogolani
3 years
"Kipimo cha wema wako si kuwarudishia wema waliokufanyia wema bali kuwafanyia wema usiowajua wala wasiokudai wema." ~ Togolani Mavura.
Tweet media one
35
279
1K
@SikilizaTogolan
SikilizaTogolani
3 years
Nasaha za Mheshimiwa Balozi @tonytogolani leo siku ya kwanza ya Mwaka Mpya.
Tweet media one
39
234
1K
@SikilizaTogolan
SikilizaTogolani
3 years
Umri unadanganya sana. Usihadaike, kinachoimarisha watu ni mapito yao si umri wao. Wapime watu kwa mapito yao si umri wao. ~Togolani Mavura.
Tweet media one
38
297
1K
@SikilizaTogolan
SikilizaTogolani
3 years
Ukitaka kuishi kwa furaha na amani: kwanza, punguza matarajio juu ya watu. Pili, wajibika zaidi kwa matatizo yako na mambo yahusuyo furaha yako. Huwezi kuangushwa wala kuumizwa na kitu usicho na matarajio nacho au mtu usiye na matarajio naye. ~Togolani Mavura.
Tweet media one
76
363
1K
@SikilizaTogolan
SikilizaTogolani
2 years
"Hakuna Dini iliyo kuu kama Upendo". ~Togolani Mavura.
Tweet media one
50
208
1K
@SikilizaTogolan
SikilizaTogolani
2 years
"Kama konokono na kobe nao waliiwahi safina basi mbio sio njia pekee ya kuyawahi mafanikio yako." ~Togolani Mavura.
Tweet media one
57
272
1K
@SikilizaTogolan
SikilizaTogolani
10 months
"Nyuma ya mafanikio ya mtu kuna ujasiri na maumivu." ~Togolani Mavura.
Tweet media one
38
264
1K
@SikilizaTogolan
SikilizaTogolani
3 years
Nasaha za Mh Balozi @tonytogolani siku ya leo.
Tweet media one
42
219
1K
@SikilizaTogolan
SikilizaTogolani
2 years
"Furaha yako ni kero kwa wengine, mateso yako ni furaha kwa wengine. Furahi kwa sauti ndogo, teseka kwa sauti kubwa. Watakuvumilia ukiteseka kwa sauti kubwa lakini sio ukifurahi kwa sauti kubwa." ~Togolani Mavura.
Tweet media one
65
295
1K
@SikilizaTogolan
SikilizaTogolani
3 years
"Mafanikio ya Mtu hutegemea Karama yake, Kadri yake na Kudra yake".
Tweet media one
39
256
1K
@SikilizaTogolan
SikilizaTogolani
3 years
Sifa za uhakika ni zile tu unazopewa usipokuwepo au ukiondoka ulipokuwepo. Zile unazopewa ukiwepo usizibebe jumla jumla zichuje. ~Togolani Mavura.
Tweet media one
40
281
1K
@SikilizaTogolan
SikilizaTogolani
3 years
"Sadaka huanzia moyoni na si mfukoni. Toa kwa sababu moyo wako umeguswa na si kwa sababu mfuko wako umefurika. Sadaka yako haitapimwa kwa kiasi bali kwa imani".~Togolani Mavura
Tweet media one
49
275
1K
@SikilizaTogolan
SikilizaTogolani
3 years
"Mungu si wako peke yako, ukikosa wewe maana yake kapata mwenzako". ~Togolani Mavura.
Tweet media one
43
234
1K
@SikilizaTogolan
SikilizaTogolani
2 years
"Kushinda si lazima mwingine ashindwe, kupata si lazima mwingine akose, kufurahi si lazima mwingine aumie.Kila mmoja hupata kilicho Kadri yake." ~Togolani Mavura.
Tweet media one
36
253
1K
@SikilizaTogolan
SikilizaTogolani
2 years
"Mungu si wako peke yako, ukikosa wewe maana yake kapata mwenzako". ~Togolani Mavura.
Tweet media one
36
199
1K
@SikilizaTogolan
SikilizaTogolani
2 years
"Haki yako idai, fadhila iombe."~Togolani Mavura.
Tweet media one
41
215
1K
@SikilizaTogolan
SikilizaTogolani
3 years
"Udhaifu haufichiki. Unasitirika tu."~Togolani Mavura
Tweet media one
30
210
1K
@SikilizaTogolan
SikilizaTogolani
2 years
"Rizki inatembea. Watu hutembea na rizki. Watu ni rizki. Tembea ukutane na watu. Watu wakukutanishe nayo." ~Togolani Mavura.
Tweet media one
39
237
1K
@SikilizaTogolan
SikilizaTogolani
2 years
"Panapo haja, maarifa huja." ~Togolani Mavura.
Tweet media one
32
200
1K
@SikilizaTogolan
SikilizaTogolani
2 years
"Ni vizuri kuwa na fedha na vitu vinavyonunuliwa na fedha,ni muhimu sana kutopoteza vile ambavyo fedha haiwezi kununua ambavyo ni imani,afya,upendo na utu." ~Togolani Mavura.
Tweet media one
53
228
1K
@SikilizaTogolan
SikilizaTogolani
2 years
"Kipimo cha kujua sasa umekuwa mtu mzima ni pale ambapo idadi ya wanaokulilia shida wewe inaongezeka wakati idadi ya wewe unaoweza kuwalilia shida inatoweka. Yakikufika pokea kwa moyo mkunjufu, yanakujaga na baraka zake." ~Togolani Mavura.
Tweet media one
46
254
1K
@SikilizaTogolan
SikilizaTogolani
2 years
"Mwenyezi Mungu hafelishi mtu, akikupa mtihani basi jua una majibu yake tayari." ~Togolani Mavura.
Tweet media one
37
176
1K
@SikilizaTogolan
SikilizaTogolani
3 months
"Katika sala unazoziomba kila siku usiache kuomba Mungu akukutanishe na watu watakaovumilia safari ya mapito yako." ~Togolani Mavura.
Tweet media one
55
247
1K
@SikilizaTogolan
SikilizaTogolani
5 months
"Wakikuomba pesa ili wakupime upendo wako, na wewe wanyime ili uwapime uvumilivu wao." ~Togolani Mavura.
Tweet media one
66
248
1K
@SikilizaTogolan
SikilizaTogolani
3 years
"Usipuuzie vijitabia vidogovidogo vya maudhi anavyovionesha mtu kwako maana ukweli wa mtu uko katika vijitabia vidogodogo vinavyomponyoka bila kutarajia na si katika mambo makubwa anayojinasibisha nayo." ~Togolani Mavura.
Tweet media one
47
296
1K
@SikilizaTogolan
SikilizaTogolani
2 years
"Mwenyezi Mungu ameficha katika macho ya binadamu mambo 3, umri, rizki na kiama. Hatujui tutaishi miaka mingapi, hatujui rizki yetu ya kesho na hatujui mwisho wetu na maisha yetu akhera yatakuwaje. Hekima yake ni tuwe wanyenyekevu." ~Togolani Mavura.
Tweet media one
47
277
1K
@SikilizaTogolan
SikilizaTogolani
10 months
"Kipimo cha wema wako si kuwarudishia wema waliokufanyia wema bali kuwafanyia wema usiowajua wala wasiokudai wema". ~Togolani Mavura.
Tweet media one
38
231
1K
@SikilizaTogolan
SikilizaTogolani
3 years
"Watoto wote wanapatikana kwa kudra za Mwenyezi Mungu tu na wala si juhudi za wazazi. Hakuna wa ndani, nje, wala haramu. Mtoto ni mtoto tu. Wote wanastahili utu na kuthaminiwa. Walipatikanaje, hilo haliwahusu watoto na wala si tatizo Lao". ~Togolani Mavura.
Tweet media one
48
254
1K
@SikilizaTogolan
SikilizaTogolani
2 years
"Usijihesabie umekuwa mtu mzima mpaka utakapoelewa kuwa maisha binafsi ya watu wengine na faragha zao hayakuhusu, wala imani zao na mitizamo yao hailazimiki kufanana na yako. Utu uzima ni hekima ya kuishi na watu usiofanana nao." ~Togolani Mavura.
Tweet media one
49
259
1K
@SikilizaTogolan
SikilizaTogolani
2 years
"Mafanikio hujengwa juu ya msingi wa mseto wa jasho, maumivu, huzuni na ibada." ~Togolani Mavura.
Tweet media one
40
173
1K
@SikilizaTogolan
SikilizaTogolani
9 months
"Nusu ya thamani ya uzuri wa kitu inapungua pale tu unapokipata." ~Togolani Mavura.
Tweet media one
27
213
1K
@SikilizaTogolan
SikilizaTogolani
2 years
"Ni heri utingwe na majukumu kuliko usiwe nayo. Majukumu hutuepusha na shari na mitihani mingi ya maisha na hutufungulia riziki. Usipotingwa nayo, utakuwa na muda mwingi wa kuhangaika na maisha ya wengine. Itakugharimu. Shukuru Mungu unayo". ~Togolani Mavura.
Tweet media one
34
262
1K
@SikilizaTogolan
SikilizaTogolani
10 months
"Kila hali katika maisha ni mtihani." ~Togolani Mavura.
Tweet media one
26
171
997
@SikilizaTogolan
SikilizaTogolani
11 months
"Mjini njoo na ujasiri, fursa utakutana nazo hukuhuku." ~Togolani Mavura.
Tweet media one
26
192
1K
@SikilizaTogolan
SikilizaTogolani
10 months
"Nidhamu, bidii na ibada havijawahi kumtupa mkono yoyote aliyevikumbatia katika maisha." ~Togolani Mavura.
Tweet media one
35
242
1K
@SikilizaTogolan
SikilizaTogolani
1 year
"Siku wote tukifanana, maisha yatakosa ladha". ~Togolani Mavura.
Tweet media one
41
218
982
@SikilizaTogolan
SikilizaTogolani
3 years
"Tunaamka kuhangaika tena sababu bado tuna chembe ya tumaini kuwa leo yaweza kuwa bora kushinda jana na hata tusipofanikiwa leo, pengine tutafanikiwa kesho. Katika maisha, poteza vyote lakini usipoteze matumaini. Ukipoteza matumaini, umepoteza sababu ya kuishi." ~Togolani Mavura
Tweet media one
51
270
966
@SikilizaTogolan
SikilizaTogolani
3 years
"Kuwapa maarifa wengine hakukupunguzii maarifa yako uliyonayo bali huyaongeza. Maarifa unayoyatoa kwa wengine yanaachia nafasi katika ubongo wako wa kuruhusu maarifa mapya. Usipoyatoa kwa wengine, hayo uliyonayo yanachakaa."
Tweet media one
35
243
960
@SikilizaTogolan
SikilizaTogolani
2 years
"Kituo kabla ya Stendi Kuu ya Mafanikio huitwa Mitihani." ~Togolani Mavura.
Tweet media one
27
215
964
@SikilizaTogolan
SikilizaTogolani
2 years
"Ukitaka kuishi maisha ya amani na furaha kwenye maisha, kubali mengine yakupite." ~Togolani Mavura.
Tweet media one
32
210
959
@SikilizaTogolan
SikilizaTogolani
3 years
"Wanafiki hawakwepeki. Wamekuwapo na watakuwapo na wametajwa kwenye vitabu vya dini. Ukibahatika kuwajua, jikaushe. Mnafiki unayemjua anaweza kukusaidia kumjua mnafiki wako usiyemjua. Utafaidika zaidi ukijifunza kuishi kinafiki na wanafiki." ~Togolani Mavura
Tweet media one
55
288
950
@SikilizaTogolan
SikilizaTogolani
2 years
"Ukipata cheo mahala papya, watakaokulaki mapema ni wafitini na walalamishi. Hawa watakusimulia mabaya tu kuhusu watu waliopo badala ya masuala. Wema na wachapakazi utawafahamu baadae kwa kazi zao. Wasikilize kwa tahadhari kubwa." ~Togolani Mavura.
Tweet media one
40
223
944
@SikilizaTogolan
SikilizaTogolani
2 years
"Usimpotee Mungu wako wakati wa neema maana naye atakupotea siku ukiwa unamtafuta wakati wa dhiki." ~Togolani Mavura.
Tweet media one
30
200
942
@SikilizaTogolan
SikilizaTogolani
1 year
"Aliyebuni saa na kalenda naye kaumbwa na Mungu iweje basi subira yako kwa Mungu uifungamanishe na saa na kalenda aliyotengeneza mwanadamu." ~Togolani Mavura.
Tweet media one
27
206
959
@SikilizaTogolan
SikilizaTogolani
1 year
"Ukipata bahati ya kuanza na kazi ya ndoto yako mshukuru Mungu maana wengi huanza na kazi inayopatikana au iliyopo." ~Togolani Mavura.
Tweet media one
27
224
949
@SikilizaTogolan
SikilizaTogolani
2 years
"Kila nyavu ina samaki wake. Nyavu ya kibua huvulii dagaa, vivyo hivyo ya jodari huvulii kibua.Utavua wale wanaotosha ukubwa wa nyavu zako. Sote tunakwenda kuvua bahari moja, tunarudi na samaki tofauti. Kabla ya kuona wivu kwa alichovua mwenzako, hangaika na aina ya nyavu yako".
Tweet media one
48
248
936
@SikilizaTogolan
SikilizaTogolani
3 years
"Wenye kufurahia maisha ni wale wanaodunduliza mafanikio madogo madogo katika kila hatua ya maisha yao huku wakiyaendea yale mafanikio makubwa kuliko wale wanaoyasubiri mafanikio makubwa sana mwishoni ambayo huenda yasitokee". ~Togolani Mavura.
Tweet media one
31
241
934
@SikilizaTogolan
SikilizaTogolani
2 years
"Ukitamani usichohitaji utapata usichotaka. Ukithamini ulichonacho utaongezewa unachohitaji. Ni rahisi kupata unachohitaji kuliko unachotaka!." ~Togolani Mavura.
Tweet media one
30
217
930
@SikilizaTogolan
SikilizaTogolani
3 years
"Subra peke yake ni mtihani kuliko mtihani wenyewe unaokusubiri." ~Togolani Mavura
Tweet media one
25
189
919
@SikilizaTogolan
SikilizaTogolani
2 years
"Wengine huonekana wazuri na wema sababu tu hawajajaribiwa na ama mapenzi, pesa au madaraka." ~Togolani Mavura.
Tweet media one
31
198
938
@SikilizaTogolan
SikilizaTogolani
2 years
"Kuna vyeo vyenye Madaraka, kuna vyeo vyenye Mamlaka na kuna vyeo vyenye Ushawishi tu. Usipojua mipaka ya madaraka, mamlaka na ushawishi utajikuta katika matatizo na lawama." ~Togolani Mavura.
Tweet media one
36
211
935
@SikilizaTogolan
SikilizaTogolani
1 year
"Vyote ni mali ya Mungu, akichukua chochote, Shukuru, hata kama ni mwili wako, basi akikuacha hai muombe asichukue ulimi tu ili uweze kulitaja na kulisifu jina lake."~Togolani Mavura.
Tweet media one
31
216
944
@SikilizaTogolan
SikilizaTogolani
2 years
"Tunamuomba mungu tunachotaka na tunachohusudu yeye hutupa tunachohitaji, kilicho kadri yetu na kilicho na heri nasi." ~Togolani Mavura.
Tweet media one
28
183
937
@SikilizaTogolan
SikilizaTogolani
2 years
"Mwenyezi Mungu hulipa wale waliotutendea uovu kwa kipimo chake, si kwa kipimo chetu." ~Togolani Mavura.
Tweet media one
38
197
925
@SikilizaTogolan
SikilizaTogolani
1 year
"Wakati ukifika, wepesi nao hukufikia!" ~Togolani Mavura.
Tweet media one
28
178
931
@SikilizaTogolan
SikilizaTogolani
2 years
"Watoto wa kwanza (first born) wanabebeshwa na kubeba mizigo mikubwa ya wajibu na lawama. Matarajio makubwa ya familia juu yao yanawabebesha wajibu, na wanaposhindwa kuyafikia matarajio hayo wanabebeshwa mzigo wa lawama. Mwenyezi Mungu awabariki na kuwawekea wepesi."
Tweet media one
80
199
925
@SikilizaTogolan
SikilizaTogolani
9 months
"Wenye roho nzuri hawadhulumiki na wanapata kadri wanavyotoa."~Togolani Mavura.
Tweet media one
25
193
927
@SikilizaTogolan
SikilizaTogolani
2 years
"Wako wanaonza maisha kwa kufyeka pori, wako wanaoanzia kwenye shamba lililotayarishwa, na wako wanaoanzia kwa kuvuna mazao yaliyokwishapandwa na wazazi. Wengine wao ndio baba wa mafanikio,wengine ni watoto wa mafanikio na wengine wajukuu wa mafanikio.Mchezo mmoja, ligi tofauti!"
Tweet media one
49
242
914
@SikilizaTogolan
SikilizaTogolani
9 months
"Likuepukalo una kheri nalo." ~Togolani Mavura.
Tweet media one
18
179
921
@SikilizaTogolan
SikilizaTogolani
2 years
"Ukiwa mwepesi kusalimu, kusema tafadhali, kusema naomba, kusema asante,kusema samahani, kusema haidhuru na kusema inatosha, utaishi vizuri na yoyote,popote maisha yatakapokupeleka." ~Togolani Mavura.
Tweet media one
42
228
916
@SikilizaTogolan
SikilizaTogolani
3 years
Kesho ni ufunguo wa mlango wa uwezekano wa mambo yote maishani. Kama kesho ipo na ukijaaliwa kuwepo, basi na uwezekano wa lolote upo. Wewe usiache ombea kesho yako tu. ~Togolani Mavura.
Tweet media one
28
221
902
@SikilizaTogolan
SikilizaTogolani
2 years
"Heshimu chaguo la mtu. Kila mtu ana mtu wake, kila muonekano una mvuto wake, kila umbile lina tunu yake na kila hulka ina mwenziwe. Hakuna aliye mbaya kwa wote, mzuri kwa wote au mwenye kumfaa yoyote. Kila mtu na maradhi yake." ~Togolani Mavura.
Tweet media one
39
240
911
@SikilizaTogolan
SikilizaTogolani
10 months
"Mwenyezi Mungu mara nyingi hukukosesha unachokitaka na hukupa unachokihitaji." ~Togolani Mavura.
Tweet media one
23
194
925
@SikilizaTogolan
SikilizaTogolani
2 years
"Tenga muda kwa ajili ya kutafakari na kujitathmini (meditation), na tenga muda kwa ajili ya kufunga (fast). Haya mawili hukuimarisha nafsi na kukupa unyenyekevu. Ndio siri ya mafanikio ya Mitume na Watu Bora." ~Togolani Mavura.
Tweet media one
37
244
908
@SikilizaTogolan
SikilizaTogolani
3 years
"Nafsi na roho yako ikisita usiipuuzie, wasiwasi ndio akili, usipuuzie ile sauti ndogo moyoni inayokukataza,yaweza kuwa salama na nusra yako." ~Togolani Mavura
Tweet media one
41
217
896
@SikilizaTogolan
SikilizaTogolani
3 years
"Hata kama unamjua mtu, ukikuta foleni panga foleni, ukiiruka unamuweka huyo unayemjua katika wakati mgumu dhidi ya walioko kwenye foleni. Mpe nafasi huyo unayemjua atafute njia bora ya kukusaidia isiyokwaza watu. Ukiondoka yeye atabaki nao". ~Togolani Mavura.
Tweet media one
41
198
903
@SikilizaTogolan
SikilizaTogolani
10 months
"Binadamu mara nyingi ni rahisi sana kubeza na kukejeli kuliko kujifunza." ~Togolani Mavura.
Tweet media one
21
193
917
@SikilizaTogolan
SikilizaTogolani
2 years
"Katika maisha, usijisahau na kufurahia sana kufanikiwa maana kufanikiwa ni tukio tu katika maisha, changamoto kubwa ni kuendelea kufanikiwa na kuishi maisha ya mafanikio." ~Togolani Mavura.
Tweet media one
19
221
890
@SikilizaTogolan
SikilizaTogolani
3 years
"Mbali ni kituo kabla ya mwisho. Wengi huchoka wakifika mbali. Hapo mbali ndipo jitihada na ndoto nyingi za wale wenye kukata tamaa zinapoishia. Wanaofanikiwa ni wenye ujasiri wa kupavuka hapo mbali. Mafanikio huwa yako mwisho". ~Togolani Mavura.
Tweet media one
33
260
891
@SikilizaTogolan
SikilizaTogolani
2 years
"Usiwe mwepesi wa kuomba halafu mgumu wa kushukuru." ~Togolani Mavura.
Tweet media one
21
166
891
@SikilizaTogolan
SikilizaTogolani
2 years
"Maumivu yaweza kuwa njia ya wokovu au mwanzo wa makovu." ~Togolani Mavura.
Tweet media one
25
164
902
@SikilizaTogolan
SikilizaTogolani
2 years
"Ukiona umeomba kwa Mwenyezi Mungu msaada na haupati majibu, jua kuwa hiyo shida bado iko ndani ya uwezo wako kuitatua. Ukimya wa Mwenyezi Mungu nao ni jibu." ~Togolani Mavura.
Tweet media one
31
167
900
@SikilizaTogolan
SikilizaTogolani
3 years
Kwa udhaifu wetu, tunatenda dhambi kila siku iwe kwa kuwaza, kwa kunena, kwa kutenda au kwa kutotimiza wajibu. Ili kufidia, tujitahidi kutimiza japo ibada moja na kutenda wema kwa mmoja kwa siku kila siku kusawazisha dhambi zetu. ~Togolani Mavura.
Tweet media one
25
220
880
@SikilizaTogolan
SikilizaTogolani
2 years
"Kwa kuwa kila kinachozaliwa hufa, basi hatukuzaliwa ili tufe, tumezaliwa ili tutimize wito wetu katika kipindi tunachojaliwa kuishi duniani." ~Togolani Mavura.
Tweet media one
22
182
890
@SikilizaTogolan
SikilizaTogolani
2 years
"Ukimya haunukuliki". ~Togolani Mavura.
Tweet media one
29
151
888
@SikilizaTogolan
SikilizaTogolani
2 years
"Kifo si foleni ya umri kwamba aliyetangulia kuzaliwa atatangulia kufa.Jiandae wakati wote na ishi maisha yote uwezavyo katika kila siku unayojaliwa kuishi. Ahirisha kila kitu isipokuwa ibada. Leo ndio siku uliyonayo, kesho ni ahadi tu." ~Togolani Mavura.
Tweet media one
44
228
892
@SikilizaTogolan
SikilizaTogolani
2 months
"Ukiishi katika jamii iliyojaa watu wenye husda, lia hadharani, furahi sirini." ~Togolani Mavura.
Tweet media one
37
224
900
@SikilizaTogolan
SikilizaTogolani
1 year
"Mwanga mdogo wa mshumaa hufukuza kiza kinene. Usipuuze na kudharau udogo wa sauti yako." ~Togolani Mavura.
Tweet media one
23
164
890
@SikilizaTogolan
SikilizaTogolani
3 years
"Usiache kumsaidia mtu kwa kudhani tu kwamba msaada wako mdogo hauwezi kutatua shida yake ya muda mrefu. Nafuu ya japo ya siku moja ni ahueni kubwa kwa mwenye shida maana shida haizoeleki bali inahimilika tu." ~Togolani Mavura
Tweet media one
33
192
871
@SikilizaTogolan
SikilizaTogolani
2 years
"Usiandike kitu mtandaoni kama hamna kesho, usiandike kama uko faraghani, daima kumbuka mitandao ya kijamii ni hadhara na wino wake haufutiki. Fikiri,tafakari kisha andika." Togolani Mavura.
Tweet media one
40
217
884
@SikilizaTogolan
SikilizaTogolani
2 years
"Kuna walioletwa duniani kuwa mbegu, kuna walioletwa kuwa mizizi, wengine kuwa mashina, na wengine kuwa matunda, wengine matawi ya kivuli, na wengine kuwa kuni. Tambua nafasi yako, wito wako na wakati wako. Ishi wito wako." ~Togolani Mavura.
Tweet media one
43
214
874
@SikilizaTogolan
SikilizaTogolani
2 years
"Usipopewa rizki kubwa unaepushwa pia na makubwa." ~Togolani Mavura.
Tweet media one
28
165
876
@SikilizaTogolan
SikilizaTogolani
3 years
"Ukiwa nacho watakusakama kuwa unaringa, usipokuwa nacho watakusakama kwa masimango. Maumivu ni madogo ukisakamwa kwa kuwa nacho kuliko kusakamwa na masimango ya kutokuwa nacho".~Togolani Mavura.
Tweet media one
28
212
865
@SikilizaTogolan
SikilizaTogolani
1 month
"Maji hayasahau mkondo wake. Vivyo hivyo pia rizki. Palipowahi kupita rizki, ni rahisi rizki kupita hapo tena." ~Togolani Mavura.
Tweet media one
25
196
886
@SikilizaTogolan
SikilizaTogolani
2 years
"Binadamu hutofautiana wako ambao shida huwafunza na wako ambao shida huwashupaza na kuwapa usugu." ~Togolani Mavura.
Tweet media one
30
193
863
@SikilizaTogolan
SikilizaTogolani
3 years
"Ukiwa kijana tambua umebeba dhamana na wajibu wa kizazi kizima. Ndio maana akikosea kijana mmoja lawama wanapewa vijana wote, Lakini akikosea Mzee mmoja lawama haiendi kwa wazee wote." ~Togolani Mavura
Tweet media one
31
223
860
@SikilizaTogolan
SikilizaTogolani
11 days
"Tunaunganishwa na dhiki na tunatenganishwa na neema." ~Togolani Mavura.
Tweet media one
34
204
899
@SikilizaTogolan
SikilizaTogolani
2 years
"Ukishindwa kuwa na utajiri wa mali na pesa basi hakikisha unakuwa na utajiri wa ndugu na marafiki wanaoweza kukufanyia yale ambayo pesa na mali vinaweza kukufanyia. Umasikini mkubwa ni kukosa vyote, yaani, pesa na mtandao." ~Togolani Mavura.
Tweet media one
35
209
864
@SikilizaTogolan
SikilizaTogolani
3 years
"Maisha huwatunuku fungu jema wale wenye kujifunza, kuelewa na kufaulu mtihani wa rizki, subra na wakati." ~Togolani Mavura
Tweet media one
25
206
859
@SikilizaTogolan
SikilizaTogolani
3 months
"Kwenye maisha mnaweza kuwa rika moja, mkafanya kazi pamoja, mkapambana pamoja ila kudra za Mungu ndio zitaamua yupi ayatangulie mafanikio na yupi awe wa mwisho kuyafikia." ~Togolani Mavura.
Tweet media one
30
217
874
@SikilizaTogolan
SikilizaTogolani
2 years
"Ustaarabu,Uvumilivu,Ukomavu, Hekima,Busara,Heshima, Kuvumiliana ni mambo ambayo hayaigiziki." ~Togolani Mavura.
Tweet media one
31
194
869
@SikilizaTogolan
SikilizaTogolani
2 years
"Kwenye kuposa na kujadiliana mahari wanakwendaga wachache ila kwenye harusi wanakuja wengi. Ndivyo maisha yalivyo, utahangaika na wachache ukifanikiwa watakujalia wengi. Iko hivyo na itabaki kuwa hivyo. Kubaliana tu na hali halisi." ~Togolani Mavura.
Tweet media one
43
205
859
@SikilizaTogolan
SikilizaTogolani
2 years
"Hakuna mwaka mrefu wala mfupi. Urefu au ufupi wake unategemeana na matukio unayokutana nayo, unayoyapitia na majukumu unayokabiliana nayo." ~Togolani Mavura.
Tweet media one
32
150
856
@SikilizaTogolan
SikilizaTogolani
2 years
"Si kila mnyama anawindwa kwa kukimbizwa, wengine wanategwa na wengine wananyatiwa. Ndivyo ilivyo pia katika maisha, si kila riziki inapatikana kwa kukimbizwa, riziki nyingine hutegwa, na nyingine zinanyatiwa." ~Togolani Mavura.
Tweet media one
24
202
849
@SikilizaTogolan
SikilizaTogolani
2 years
"Fikiri Pekeyako, Amua Pekeyako, Tenda na Wenzako." ~Togolani Mavura.
Tweet media one
25
167
840
@SikilizaTogolan
SikilizaTogolani
2 years
"Kila mtu atafanikiwa kwa uhakika na kikamilifu kupitia talanta na wito wake.Kwanza tambua talanta na wito wako na mengine yote yatajipa." ~Togolani Mavura.
Tweet media one
31
165
846
@SikilizaTogolan
SikilizaTogolani
2 years
"Kama hauko tayari kuelewa kwa usia, mawaidha, maapizo na makanyo, dunia inao watu wengi wa kutosha walio tayari kukuelewesha kwa maumivu na vitendo." ~Togolani Mavura.
Tweet media one
33
209
846
@SikilizaTogolan
SikilizaTogolani
9 months
"Watu wengi hukosa kufanikiwa pamoja na uwezo wao mkubwa sababu ya kukosa unyenyekevu na utii." ~Togolani Mavura.
Tweet media one
20
189
858
@SikilizaTogolan
SikilizaTogolani
2 years
"Usimsimange mwenye shida wala kumuadhibu ambaye tayari ameadhibiwa na maisha.Kama huwezi kumtua mzigo wake basi usimtwike zaidi. Lawama yake itakuwa kubwa kwako uliyemuongezea mzigo mdogo kuliko yule aliyembebesha mzigo mkubwa" ~Togolani Mavura.
Tweet media one
27
230
849
@SikilizaTogolan
SikilizaTogolani
2 years
"Usiruhusu Upendo na Chuki vikazidi akili na ufahamu wako. Ukipenda penda kwa kiasi ukichukia chukia kwa kiasi." ~Togolani Mavura.
Tweet media one
41
201
855