mocu_official
@MoCU_Official
Followers
85
Following
4
Media
427
Statuses
564
Official page of Moshi Co-operative University Instagram page: mocu_official_page
Kilimanjaro, Tanzania
Joined September 2023
Ziara hiyo inalenga kutathmini maendeleo ya KICoB na kukagua ujenzi wa majengo ya Kitaaluma na bweni la wanafunzi, ambao unafadhiliwa na Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET)
0
0
0
Naibu katibu Mkuu Sayansi, Teknolojia na Elimu ya Juu, Prof. Daniel Mushi amefanya ziara katika Taasisi ya Elimu ya Ushirika na Biashara Kizumbi (KICoB) . .
1
0
1
Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Prof Alfred Sife amefungua mafunzo ya kuwaingiza watumishi wapya kazini "Orientation", huku akisisitiza waajiriwa hao kuifahamu dira, dhima na ushirika kwa kina. Mafunzo hayo yatakayofanyika kwa siku mbili yameanza leo 21 Mei, 2025.
0
0
0
Viongozi mbalimbali wa vyama vya ushirika na taasisi za kijamii wakiendelea na mafunzo ya kuwajengea uwezo kwa siku ya tatu. Mafunzo hayo yanatolewa na wawezeshaji kutoka MoCU kwa ufadhili wa @weeffect
0
0
0
Picha mbalimbali za kikao cha Manaibu Makamu Wakuu wa Vyuo-Taaluma,Utafiti na Ushauri Elekezi. Kikao kimefanyika leo katika kampasi kuu Moshi.
0
0
0
Picha mbalimbali zikiangazia Kikao cha Manaibu wa Makamu Mkuu wa Chuo wanaoshughulikia masuala ya utawala. Kikao hicho kimefanyika leo 19 Mei, 2025
0
0
0
Ugeni kutoka Chuo cha York Canada umetembelea MoCU lengo likiwa ni kushirikiana na Chuo ili kuweza kuleta wanafunzi wa "MBA executive program" kwenye mafunzo kwa vitendo hususani katika vyama vya ushirika @YorkUniversity
0
0
0
Picha mbalimbali zikionesha viongozi wa Vyama vya Ushirika na taasisi mbalimbali za kijamii wakipatiwa mafunzo ya kuwajengea uwezo yanayotolewa na wawezeshaji kutoka MoCU. Mafunzo hayo yatatolewa kwa muda wa siku tano kuanzia leo na yanafadhiliwa na @weeffect
0
0
0
Picha mbalimbali zikiangazia tukio la fani,vipaji na ubunifu yaani "career fair" kwa siku ya kwanza. Tukio hilo linalohusisha mafunzo ya nadharia,vitendo pamoja na maonesho ya bidhaa, linatoa fursa ya kuwakutanisha wanafunzi pamoja na waajiri.
0
0
0
wadau mbalimbali wametembelea mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET) unaoendelea katika Taasisi ya Elimu ya Ushirika na Biashara Kizumbi (KICoB). Majengo yanayojengwa ni “Academic Complex na Hostel”
0
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha akiambatana Katibu Tawala, Mkuu wa Wilaya, MKurugenzi wa Manispaa, Diwani, timu ya ulinzi na usalama na
1
0
0
Mafunzo hayo yamefanyika mchana wa leo (14/05/2025) kwa kuongozwa na Jeshi la Zima moto na Uokoaji mkoani Shinyanga.
0
0
0
Watumishi wa Taasisi ya Elimu ya Ushirika na Biashara Kizumbi wamejengewa uwezo juu ya kujikinga na moto unaoweza kuleta madhara ofisini, nyumbani na kwenye vyombo vya usafiri.
1
0
1
Picha mbalimbali zikionesha matukio ya uzinduzi wa ligi ya wanafunzi kimadarasa Katika ligi hiyo inayodhaminiwa na benki ya Azania Michezo mbalimbali itashindaniwa ikiwa ni pamoja na mpira wa miguu, mpira wa pete, kikapu na mpira wa wavu
0
0
2
Picha mbalimbali zikionesha matukio ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi wakionesha vipaji vyao katika jukwaa la Silent Ocean UNI Awards Kilimanjaro 2025.
0
0
1
Picha mbalimbali zikionesha viongozi wa Chama Kikuu cha Ushirika TANECU kutokea Mtwara wakipokea vyeti,mara baada ya kupata mafuzo ya elimu ya Ushirika yaliyoandaliwa na Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi (MoCU).
0
0
1
Pichani ni viongozi wa Chama Kikuu cha Ushirika cha TANECU kutokea Mtwara wakila kiapo cha maadili, mara baada ya kumaliza mafunzo ya Ushirika yaliyoandaliwa na Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi (MoCU).
0
0
2
Picha mbalimbali zikionesha matukio ya viongozi wa Chama Kikuu cha Ushirika TANECU kutokea Mtwara wakifanya ziara ya mafunzo taasisi tofauti tofauti ikiwemo KNCU.
0
0
0