
Dazzy Elly
@AsajileDaniel
Followers
9K
Following
604K
Media
17
Statuses
301K
Hustling is my favorite game.
Mbeya, Tanzania
Joined December 2023
Palipo na haki huna haja ya kuhubiri amani,huwa inakuja yenyewe tu.Ukiminya haki basi automatically amani inapotea,ajabu kwetu waminya haki ndio wanaohubiri amani. Huhitaji ushawishi katika kutumia akili yako vizuri,unahitaji ukweli tu,ukweli humuweka mtu huru. Good morning fam.
41
33
64
Kuna uwezekano kabisa moyo ukachoka kumpenda yule mtu uliyedhani atakua wa maisha yako yote. Ikikukuta hiyo hali kaa chini na mwenza wako mpeane ukweli,jela ya mapenzi ni mbaya mno,inafupisha maisha. Moyo ndio kila kitu,ukichoka huwezi ulazimisha wala kuuamsha. Good morning fam.
2
4
11
OODAcon is diving deep into today's geopolitical and technological dynamics including sessions some of the nation's greatest experts in AI and Cyber. We hand selected the right experts in PRC economic, military and industrial intentions. Hear from the Special Assistant to the
0
5
11
Fuatilia hili,jinsi mtu anavyopata elimu ndio uwezekano wa kutajirika unavyokua mdogo yani matajiri wengi ni wale wasio na elimu kabisa au wenye elimu ndogo. Tunatumia mfumo wa elimu ya mkoloni,tunalishwa ujinga ili tuendelee kutawalika. Elimu bure ila ni sumu ya ubongo. Gm fam.
27
22
52
Kuna zile mbinu walikua wanatumia akina Nyerere,upolisi na ualimu ni kwa waliopata alama za chini. Ni mbinu za kuwaendesha kirahisi,polisi mwenye uwezo mdogo kichwani ni rahisi kufanya chochote boss wake asemacho. Waalimu shida ni uwingi wao. Nyakati zimebadilika,wao bado Gm fam
43
31
77
Wanasiasa walianza uongo,tukakubali ikawa sheria. Wakaanza rushwa,ikawa sheria. Wakaja ufisadi,ikawa sheria. Wameingia kwenye utekaji,tukikubali inakua sheria na itaonekana kawaida kabisa. Nguvu yao inatoka kwetu,wanapima akili zetu wakiona zimelala,wanahalalisha. Tuamke Gm fam.
40
23
62
Single mothers huwa wanaonewa kwa makosa ya wanaume wawili,wa kwanza aliyemtelekeza na wa pili wewe unayeamua kuwa nae,hujui kusoma mazingira.Unakuta mama anampenda sana mwanae,huo ndio upendo wa baba wa mtoto,usichoelewa hapo ni kipi? Hawezi mkazia kamwe. Gm fam.
5
7
21
Huwezi kubadili kitu chochote mpaka pale utakapoacha mazoea na kufanya kitu tofauti na unachofanya kila siku,siri ya mafanikio ipo ndani ya ratiba zako za kila siku. Matendo yanaongea kwa sauti kuliko maneno,tumekua watu wa maneno mengi mno. Tubadilike sasa. Good morning fam.
38
21
60
Powerful people act by the old testament and we judge them by the new testament. Wenye nguvu watabaki kuwa na nguvu na wanyonge watanyongwa sana.Umewahi sikia hukumu ya kesi ya mabilioni? Kama hujawahi sikia fuatilia kidogo utaona vichekesho.
2
3
16
Kitu tusichokizangatia ni kuwa nguvu ya utawala wetu inatoka kwa wananchi wenyewe. Ni mazoea mabaya na uoga ndio unaotufanya tuone kuwa hatuwezi ila kiuhalisia waamuzi wa yote ni sisi wananchi. Mfumo umechezewa ili kunufaisha wachache,unaweza kuwekwa sawa tukiamua. Gm fam.
21
11
35
Dunia ni njia na tunafanya mambo kwa hatua na katika hatua hizo kuna muda tunajisahau. Polisi anajisahau vipi kuwa yeye ni mwananchi kama mwananchi mwingine na anaishi na raia,hata kama anaishi kota kuna siku atastaafu atarudi kitaa,na wanasahau kuwa wana ndugu pia? Gm fam.
44
32
74
Initially kila mtu anazaliwa mwema,roho mbaya tunakuja kujifunzia duniani. Matendo ya watu mara nyingi yanaleta maudhi na kero kwa watu mwisho hufikia kujenga roho za chuki na visasi. Kitovu kikubwa cha uovu ni ubinafsi,kujiona wewe unastahili kuliko wengine. Good morning fam.
11
6
20
Easy come,Easy go is just a state of mind. Watu makini wakipata kitu kwa nguvu au mateso hulinda hivyo vitu visipotee na viongezeke zaidi na hata vikija kwa website hufanya hivyo hivyo. Wengi hupoteza wapatavyo kwa matumizi mabaya kwa kuwa kesho ipo. Ni akili yako tu. Gm fam.
9
5
18
Ukiangalia kwa umakini,suala la bahati humpata yule aliyetengeneza channel kwenye kitu husika,bahati haiangukii popote pale. Ni katika harakati zako ndio unaweza pata bahati,ndio mana wanasema mwenye nacho huongezewa. Jishughulishe ili kuongeza nafasi ya kubahatika. Gm fam.
51
29
71
Watu hawaogopi kufeli bali wanaogopa ile hukumu ya kimya kimya wanayopewa na watu baada ya kufeli. Watu huwa wanahukumu hata kwa yale wao wasiyoweza kuyafaulu,ndio asili ya watu. Ukiangalia watu wanahukumu vipi maana yake umefeli mara mbili,maisha ni yako. Ishi utakavyo. Gm fam.
31
27
51
Utakutana na watu wengi sana kwenye maisha yako na hata wale ambao moyo wako utapenda kuwa nao karibu na siku zote ila tabia yako ndio itaamua huo ukaribu ue wa muda gani. Tabia ni kivutio chako cha kwanza watu kukuhitaji kwenye maisha yao. That positive energy. Good morning fam
20
6
30
Kila mtu ni mstaarabu na wa maana mpaka pale atakapofungua kinywa chake au atakapoandika.Ukimya ni fumbo. Sio kila kitu lazima kisemwe na sio kila kitu cha kukalia kimya, akili yako itapimwa na muitikio wako wa jambo husika. Kuwa makini na mdomo wako. Good morning fam.
31
14
40
Kama unaweza kuepuka zile tabia zinazoleta uraibu basi ziepuke mbali kabisa, watu wanateseka sana kuziacha ili waendelee na maisha ya kawaida. Kaa mbali na nyeto,mapenzi ya jinsia moja,video za ngono na madawa yoyote.Ujana una mengi ila unaweza yakwepa hayo. Good morning fam.
47
27
64
Tuna tofauti kubwa sana. Wakati watoto wa masikini tunakaa vijiweni kubishana mpira na siasa,watoto wa matajiri wako wanapambana kujiweka kwenye nafasi za uongozi watuongoze. Masikini ni wengi kuliko matajiri,shida ni tunataka nini na umoja wetu? Good morning fam. Blessed month.
44
22
64
Kwenye ndoa,mwanaume akipata pesa atafanya maendeleo ya nyumbani kwake maana familia ndio kila kitu kwake. Mwanamke akipata pesa huwa anafanya maendeleo kwao au kwingine tu tena kwa siri. Ni imani tofauti,mwanaume anafikiri ndoa ni milele,Mwanamke anajiandaa akiachika. Gm fam.
57
36
90
Watu hodari ni wale ambao wanajua udhaifu wako na wanaishi nawe kama hakuna lolote,wanathamini uwepo wako na kila kinacholetwa na uwepo huo. Ukimpenda mtu sana,huo upendo ndio huwa udhaifu wako,watu dhaifu hutumia kuumizia,kuendeshea na kutesa watu. Just let love be love Gm fam.
54
33
74